Phiri amrudisha Kaseja Msimbazi
KOCHA Mkuu wa
Simba Mzambia, Patrick Phiri, amesema yupo tayari kufanya kazi na Juma Kaseja
katika kikosi chake kwa kuwa anamjua vizuri na kwamba ni mmoja wa magolikipa
wazuri hapa nchini.
Phiri
amelazimika kuyaweka wazi hayo baada ya kuwa na taarifa za Wekundu hao wa
Msimbazi kumrejesha kipa huyo ambaye kwa sasa anaichezea Yanga ili kuboresha
kikosi chake.
![]() |
Kaseja |
Phiri anadai kulingana na upungufu uliopo katika nafasi ya
kipa kwenye kikosi chake, hana budi kutaka kuongezewa kipa mwingine mzoefu ili
kusaidiana na waliokuwepo katika kikosi hicho.
Simba inaendelea
na mazoezi kwa ajili ya maandalizi ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, lakini
inakabiliwa na upungufu mkubwa kwenye kikosi chake kutokana na kuwa na kipa
mmoja tu kikosini, Manyika Peter, baada ya wengine wawili; Ivo Mapunda na
Hussein Shariff kutokuwepo kutokana na kukabiliwa na matatizo tofauti tofauti.
Ivo hayupo kwa
sababu anamalizia msiba wa mama yake mzazi wakati Sharrif yeye ni majeruhi.
Kutokana na hali
hiyo, Phiri amesema anahitaji kipa mwingine wa nyongeza hivyo kama uongozi
utaamua kumsajili Kaseja itakuwa furaha kwake ikizingatiwa kuwa golikipa huyo
anaujua utamaduni wa Simba kutokana na kuichezea kwa muda mrefu.
"Kaseja ni
mmoja wa wachezaji walioitumikia Simba kwa muda mrefu tena kwa mafanikio, hivyo
nathubutu kusema anaujua utamaduni wa klabu hii, kama atakuja hatutapata tabu
kwake kwani anajua kila kitu hapa," Phiri.
Phiranasema amepeleka mapendekezo ya kuongezewa kipa mwingine ili kusaidiana na waliopo
ambapo japo hakuweka wazi kwamba anamtaka Kaseja lakini amesisitiza kuwa iwapo
atakuja atafanya naye kazi, jambo ambalo linatafsiriwa kuwa bado anamuhitaji
kikosini.
Unafuu kwa Simba
unaweza kupatikana kutokana na kauli ya uongozi wa Yanga ambao ulikaririwa hivi
karibuni kupitia kwa Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano ya klabu hiyo, Seif
Ahmed 'Magari' akisema kuwa klabu hiyo haina nia ya kumzuia kipa huyo endapo
anataka kujiunga na Simba, lakini akasisitiza kuwa ni lazima taratibu zifuatwe.
Kaseja anataka
kuondoka Yanga aliyojiunga nayo kwenye usajili wa dirisha dogo la msimu
uliopita kutokana na kukosa nafasi ya kucheza, kwa vile kocha wa timu hiyo,
Marcio Maximo amekuwa akimtumia Deogratius Munishi 'Dida' kama kipa wake namba
moja.
Unaweza kutoa maoni yako hapo chini..
Maoni
Chapisha Maoni