Huruma yamponza ofisa
MAMLAKA ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Jijini Mwanza (MWAUWASA)
imemsimamisha kazi Ofisa Raslimali Watu, Zacharia Membo, kupisha uchunguzi wa tuhuma za kuajiri na
kuwalinda watumishi wasio na sifa za kupata ajira.
Uamuzi huo umefikiwa na kikao cha Bodi ya MWAUWASA kilichoongozwa
na Mwenyekiti wake, Christopher Gachuma baada ya kupokea malalamiko katika
kikao cha watumishi wa mamlaka hiyo.
Mkurugenzi Mtendaji wa MWAUWASA, Anthony
Sanga, amethibitisha kusimamishwa kwa ofisa huyo
.

Amesema hatua hiyo imechukuliwa kuupisha uchunguzi wa tuhuma
zinazomkabili baada ya kulalamikiwa na watumishi wenzake.
Taarifa za ndani toka MWAUWASA zimeeleza kuwa katika kikao hicho watumishi walilalamikia kitendo cha ofisa huyo
kuwalinda watumishi wenye vyeti bandia licha ya kuarifiwa.
Inaidaiwa ofisa huyo licha ya kutambua watumishi hao kutokuwa na
sifa bado amekuwa akiwachangisha fedha baadhi yao kuwasaidia kulinda ajira zao.
Kutokana na malalamiko hayo Gachuma alimtaka Mkurugenzi wa MWAUWASA
kumchukulia hatua kali za maadili ofisa huyo.
Amesema watumishi wote watakaobainika
kughushi vyeti nao wachukuliwe hatua ikiwamo kupendekeza kwa Waziri wa Maji
watimuliwe kazi mara moja.
Mkurugenzi Mtendaji wa MWAUWASA, Anthony
Sanga, amesema ofisa huyo anatuhumiwa
kutumia ofisi na wadhifa wake vibaya ikiwa ni pamoja na kujipatia fedha.
Maoni
Chapisha Maoni