Obama:Filamu ya Kim Jong Un ionyeshwe
Rais wa marekani Barack Obama
ameimbia Korea Kaskazini kuwa Marekani itajibu kisa ambapo wizi wa
mtandao ulioendeshwa dhidi kampuni ya filamu ya Sony Pictures hali
iliyosababisha kufutiliwa mbali kwa maonyesho ya filamu inayomdhihaki
kiongozi wa korea kaskazini kim jong- un.
Lakini mwandishi wa BBC anasema kuwa hatua hiyo haitakuwa rahisi kwa Marekani kutokana na kujitenga kwa Korea kaskazini.
Filamu ya Kumdhihaki rais wa Korea kazkazini Kim Jong Un iliozuiliwa na kampuni ya Sony Pictures kufuatia vitisho ![]() |
| Obama |
Hata hivyo Sony ilisema kuwa ilichukua uamuzi huo kwa kuwa kumbi nyingi kubwa za sinema nchini Marekani zilikataa kuonyesha filamu hiyo.
Sony imesema kuwa ina mipango wa kuionyesha filamu hiyo na kwa sasa inatafuta njia zingine za kuionyesha.-BBC

Maoni
Chapisha Maoni