Mwanamke amuua mumewe katika ugomvi wa familia
MWANAMUME mkazi wa mtaa wa Mkoani Kata ya Kalangalala
wilayani Geita, Kipara Ngw’endesha (46),
ameuawa kwa kupigwa na kitu kizito sehemu mbalimbali za mwili na mkewe kutokana
na ugomvi wa familia.
Akizungumzia
tukio hilo, mtoto wa marehemu, Regina Kipara (19), alisema tukio
hilo lilitokea juzi usiku baada
ya mke wa mwanamume huyo, Mwadawa Mussa, kumshambulia kwa kutumia mpati ambao hutumika kushikia sufuria wakati
wa kupika chakula.

Regina
alidai chanzo cha mauaji hayo ni ugomvi
wa familia uliosababishwa na hali ngumu ya maisha inayoikabili familia
yao.
“Yaani
huyu mama alikuwa akitaka kila anapotaka fedha apewe na ikitokea baba akasema
hana anaanzisha vurugu,’’alisema.
Regna alisema ilifikia kipindi baba yao
aligoma hata kumtolea mahali kwa sababu
alikuwa ni kero katika familia
hiyo.
Alisema kabla ya mauti kumkuta baba yao alikuwa na
mpango wa kuachana mama yao kutokana na
vurugu zisizokwisha alizokuwa
akizianzisha mama yao huyo wa kambo.
‘’Unajua
hali ya uchumi hapa nyumbani imeporomoka
kutokana na mikopo ambayo baba alikuwa amechukua kwenye taasisi za
fedha ndiyo maana hata mimi nimerudishwa
shule sababu ya ada na baba aliniambia nimsubiri ajipange ndiyo niendelee na
masomo yangu,”alisema.
Mwenyekiti
wa mtaa wa Mkoani ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Kalangalala mjini Geita,
Peter Donald, amethibitisha kuwapo
mauaji hayo na kwamba tayari
mwanamke huyo anashikiliwa na polisi kwa
hatua zaidi.
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Geita, Joseph alisema upelelezi wa tukio hilo unaendelea.
Maoni
Chapisha Maoni