Mshindi wa kwenda hifadhi ya Serengeri apatikana
KAMPUNI ya Bia ya Serengeti(SBL)
imempata mshindi wa kwenda hifadhi ya Taifa ya Serengeti ikiwa ni droo ya pili
tangu apatikane mshindi wa Bajaji limo kupitia shindano la kinywaji chake cha
Serengeti Premium larger la ‘Tuitoke na Serengeti’ likiwa na lengo ni
kuutangaza utalii wa ndani.
Meneja wa Bia ya Serengeti, Rugambo Rodney (katikati) akiongea na waandishi wa habari hawapo pichani wakati wa kuchezesha bahati nasibu ya shindano la Tutoke na Serengeti, linaloendeshwa na kampuni hiyo, ambapo Bw. Hassan Mfaume ameibuka mshindi katika Shindano hilo, kulia ni Msimamizi toka bodi ya michezo ya kubahatisha, Abdallah Hemedy na kushoto ni Auditor kutoka Pricewater House Coopers Ltd, Golder Kamuzora hafla hiyo imefanyika makao makuu ya Serengeti jijini Dar es Salaam.
Akizungumza Dar es Salaam leo Meneja wa SBL Rugambo Rodney amesema kuwa
mshindi huyo ni Hassan Mfaume mkazi wa Mabibo na amepata ziara ya kwenda kutembelea hifadhi ya taifa
ya Serengeti.
amesema Hassan ambaye alikua kikazi Mwanza alionekana kushangazwa
na kushitushwa baada ya kusikia taarifa kwamba amekuwa mshindi.
“Droo
hii imekuja wiki moja tu baada ya Rukia
Almasi, ambaye ni Mama wa nyumbani na mkazi wa Kihonda-Morogoro kuibuka na ushindi wa Limo Bajaj katika kampeni hii
inayoendelea yenye lengo la kuutangaza utalii wa ndani,”
Ameendelea kusema kuwa Hassan ameshinda
safari ya watu wawili iliyolipiwa gharama zote na anaruhusiwa kwenda na mwenza
wake, SBL watagharamia kila kitu kuanzia malazi, usafiri pamoja na vivutio
mbalimbali.
Hata hivyo Rodney
aliwasihi watanzania kuendelee kushiriki kwani zawadi za kushindaniwa zipo
nyingi, kampuni imelenga katika kuinua utalii wa ndani ikiwa ni njia mojawapo
ya kurudisha sehemu ya faida kwa wateja wake.
Amesema kampeni
ya ‘Tutoke na Serengeti’ wameungana na B-Pesa wataalam wa teknolojia mpya ambao
hivi karibuni wamezindua mfumo mpya wa usafirihaji wa fedha na watahusika katika kusambaza fedha kwa washindi
mbalimbali kote nchini kupitia simu za mkononi.
Maoni
Chapisha Maoni