Escrow yamletea balaa Mwenyekiti ccm
MWENYEKITI
wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Nyamagana, Raphael Shilatu na
Meneja Kampeni wa chama hicho Kata ya Igoma, Robert Itimbula, jana
walizomewa wakati wakijaribu kukitetea chama hicho kutohusika na wizi wa fedha za
akaunti ya Tegeta Escrow.
Kauli
iliyowaponza viongozi hao wa CCM ni kuzungumzia suala la uchotaji wa fedha za
Akaunti ya Tegeta Escrow na ubadhirifu wa Sh bilioni 46.5 za Halmashauri ya
Jiji la Mwanza.
Walisema
CCM haihusiki kwa njia yoyote na wizi huo bali ni watu wachache binafasi.

Dalili za
kuzomewa ilianza kuonekana mapema Itimbula alipopanda jukwaani na kujaribu
kutambua kuwapo vyama vya upinzania vilivyohudhuria kwenye
mkutano huo wa CCM kwa kuvitaja kimoja kimoja.
Alipotaja Chadema watu walilipuka kwa shangwe na vifijo huku
wakionyesha vidole juu kama ishara ya Chadema.
Tukio hilo
ambalo lilidumu takribani dakika 15 hadi kurejea utulivu, liliwafanya
viongozi hao kushindwa kuendelea kuzungumza kwa wakati huo.
Shilatu
alisema CCM itashinda kwa kishindo kwa
sababu imefanya mchujo wa wagombea wenye sifa tofauti na ilivyo kwa vyama vya
upinzani ambavyo vimewasimamisha watoto ambao hawana uwezo hata wa kusuluhisha
ndoa.
“Nataka
kuwaelezea mambo ya Escrow na ubadhirifu wa jiji letu uliosababisha kupata hati
chafu..., sasa mnapiga yowe, hapa msifanye ushabiki usio na maana… ni vema
mkasikiliza ili mpate ukweli, endeleeni na ushibiki huo ambao hautawasadia.
“Serikali
ya CCM tumejipanga kuwachukulia hatua wale wote waliohusika ndiyo maana tuliamua
kuwaweka hadharani kupitia Kamati ya Hesabu za Mashirika ya Umma (PAC) jamii
iwajue ni wabadhirifu, kukibwa nawaomba tumieni busara kufanya uamuzi sahihi
Desemba 14, mwaka huu,”alisema.
Meneja
Kampeni wa CCM, Itimbula, alisema wamebaini njama za Chadema kuwachukua
wanafunzi wa sekondari na vyuo na kuwaandikisha katika vituo mbalimbali
ili kuwapigia kura ifikapo Desemba 14 mwaka huu na kusisitiza kwamba
watawakamata kwa kuwa tayari wamewajua.
Maoni
Chapisha Maoni