DIAMOND: Nishachekwa sana kisa Lugha
BAADA ya
kurejea nyumbani na tuzo tatu mikononi zilizoamsha furaha ya Watanzania wengi,
Nyota wa muziki wa kizazi kipya Naseeb Abdul ‘Diamond Platnum’, amedai alishawahi
kuchekwa sana kisa hajui kuongea lugha ya kiingereza.
Nyota huyo
aliyasema hayo baada ya kuzinyakuwa tuzo tano na kuwataka wasanii wenzake
kuacha tabia ya uwoga na kujenga mazoea ya kutokuwa na aibu ya kuongea
kingereza hata kama hawajui ili waweze kutimiza mafanikio yao.
“Unajua mimi
nilichekwa sana ooo Diamond hajui kingereza, sasa kutokana na maneno yao mimi
nikawa najitahidi mpaka sasa naingia sehemu mbalimbali ikiwemo mjengoni ‘Big
Brothjer’, yani kwa sasa natema maneno mpaka anayenisikiliza anajisikia raha,”.
Alisema ni
wakakti wa wasanii wenzake, kuachana na tabia ya majungu, Uwoga, dharau, kasha
kutanguliza heshima mbele ili waweze kufanikisha muziki wao ufike zaidi ya
alipo yeye hivi sasa.
“Wasanii
wakiacha tabia za ajabu ajabu, muziki wa Tanzania utakuwa zaidi ya Nigeria,
lakini sasa sisi kwa sisi tunasemana wenyewe kwa wenyewe, kikubwa ni kujiamini kwa kila mmoja ili
muziki wetu usiyumba,”
Maoni
Chapisha Maoni