Chadema yataka mabadiliko

MWENYEKITI  wa chama cha  Demokrasia  na maendeleo (CHADEMA), Wilaya ya Moshi vijijini, mkoani Kilimanjaro, Ekaristi Kiwia, amewataka  makatibu
kata wa chama hicho kufanyakazi ambayo italeta mabadiliko ya chama katika ngazi ya vijiji hadi Taifa, ili kuweza kuchukua dola katika uchaguzi ujao
.
Kiwia ameyasema hayo katika uzinduzi wa kampeni za uchaguzi wa serikali za mitaa, wilaya Moshi vijijini, ambapo aliwataka makatibu wa kata na vitongoji kwenda kwa wananchi badala ya kukaa maofisini
http://upload.wikimedia.org/wikipedia/commons/b/b3/Kilimanjaro_Moshi.jpg.
Amesema lengo la chama ni kujiimarisha katika ngazi zote, makatibu wote kutoka ngazi zote za kata na vitongoji wanatakiwa kutekeleza wajibu wao ipasavyo kwa kufuata sheria na katiba ya chamaili kuleta mabadiliko ya kweli katika kuongoza dola.

“Makatibu wote katika ngazi zote, nendeni vijijini nataka wakati wowote mkalete ripoti kwa sababu viongozi wa ngazi za juu wanataka kuona mlichokifanya, hatuna muda wa kupoteza hapa ni kazi tu”
Katika hatua nyingine amewataka viongozi hao kuhakikisha kuwa wanasimamisha wagombea wadilifu ambao wanaweza kujenga heshima ya chama ambao hawapendi rushwa na kujinufaisha wenyewe.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HADITHI:MWALIMU MAGDALENA sehemu ya 1

Hadithi: Mwalimu Magdalena sehemu ya 5

Hadithi: Mwalimu Magdalena sehemu ya 4