Watu 300,000 hufariki dunia kwa kuzama kila mwaka
Ripoti iliyotolewa jana na WHO imeeleza kuwa, moja ya sababu kuu ya vifo vinavyotokea duniani ni kuzama majini watu wasiopungua laki tatu na elfu sabini na mbili kila mwaka. Ripoti ya Shirika la Afya Duniani imetaka zichukuliwe hatua madhubuti za kuzuia matukio ya kuzama majini hasa kwa vijana na kusisitiza kwamba nusu ya watu wanaozama majini ni wenye umri wa chini ya miaka 25. Ripoti hiyo imeongeza kuwa, kiwango cha watoto wanaozama walio na umri wa chini ya miaka mitano ni kikubwa mno.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Afya Duniani Margaret Chan amewataka viongozi wa nchi mbalimbali duniani kuchukua hatua madhubuti za kukabiliana na majanga ya kuzama watu majini.-Irn
Maoni
Chapisha Maoni