Waislamu Ilala kumuombea Rais Kikwete
UMOJA wa Misikiti ya Ilala jijini Dar es Salaam unatarajia
kufanya dua maalum ya kumuombea Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Jakaya Mrisho Kikwete itakayofanyika kesho alhamisi katika
msikiti wa Taqwa uliopo Ilala, Bungoni.

Dua hiyo imepangwa kufanyika kuanzia saa mbili usiku baada ya
swala ya Inshaa na masheikh mbalimbali wa umoja wa misikiti hiyo pamoja na
waumini na wageni wengine wanatarajia kuhudhuria.
Mwenyekiti wa Umoja wa
Misikiti ya Ilala Sheikh Abdul Wakati, amesema dua hiyo imelenga kumuombea Rais
Kikwete ili Mwenyezi Mungu amjaalie afya njema na kurejea katika kuwatumikia
watanzania.
“Sisi Umoja wa Misikiti ya Ilala tumeandaa dua hii maalum kwa
ajili ya kumuombea Rais wetu apate nafuu na kurejea katika ujenzi wa taifa,
tunawaomba waumini wajitokeze kwa awingi katika dua hii ili kuweza kufanikisha
azma yetu hii.”
Maoni
Chapisha Maoni