Owino: Hata sielewi nifanyeje
BEKI wa kati na nahodha wa Simba, Joseph Owino raia wa Uganda,
ametamka la moyoni na kusema inamuuma sana na anachanganyikiwa kwa
kushindwa kuamini matokeo ya ajabu ambayo klabu yake inaendelea kuyapata
ikiwa ni sare ya sita, pointi sita, mchezo wa sita na mabao sita.

Owino ndiye mfungaji wa bao pekee la mchezo wao
uliopita, waliotoka sare ya 1-1 na Mtibwa Sugar Uwanja wa Jamhuri
Morogoro. Beki huyo tegemeo kwenye kikosi hicho alisema: “Inauma sana
kuendelea kupata matokeo ya namna hii, sare ya sita.
Nashindwa kuelewa na inashangaza kinachoendelea
kutokea kwenye timu yetu, sijui ni nini lakini ndiyo hivyo,”alisema
Owino. Lakini mshambuliaji wa Mtibwa Sugar, Mussa Hassan ‘Mgosi’
alisema; “Bado wana nafasi ya kufanya vizuri kwani mechi zilizobaki ni
nyingi.”-Mwanasport
Maoni
Chapisha Maoni