Mwambusi: mizengwe,Shutuma vimeniondoka Mbeya City
SIKU chache
tu baada ya aliyekuwa Kocha Mkuu wa Mbeya City, Juma Mwambusi kuitosa timu hiyo
kwa madai ya kuchoshwa na shutuma zilizokuwa zikitolewa dhidi yake kila
kukicha,BINGWA limemsaka na kufanikiwa kuzungumza naye ili kupata undani wa
sababu zilizopelekea uamuzi wake huo.
Mwambusi ambaye alitwaa tuzo ya kocha bora ya msimu uliopita akiwa na kikosi cha Mbeya City amejikuta kwenye wakati mgumu msimu huu baada ya timu hiyo kuboronga kwenye mechi zake hivyo kujikuta ikikamata mkia.

Mbeya City
ambayo msimu uliopita ilimaliza ligi ikiwa kwenye nafasi ya tatu,imeshinda
mechi moja pekee kati ya saba ilizocheza mpaka sasa,huku ikipigwa nne na kutoka
sare mbili.-Gazeti la bingwa limeripoti
Maoni
Chapisha Maoni