Mtuhumiwa azimia mahakamani

MSHITAKIWA wa kesi ya Ubakaji ya aliyekuwa mwanafunzi wa miaka 14 wa Shule ya Msingi Ananasifu ‘A’  Thobias Dibogo (25),   amezimia  Mahakamani(Kinondoni) ambapo upande wa mashitaka ulikuwa tayari kwa ajili ya kusimamisha shahidi wa kwanza ambaye ni mama Mzazi wa msichana huyo.http://easydivorcehouston.com/wp-content/uploads/2013/10/lawyer-03.jpg

Mbele ya Hakimu Boniphace Lihamwike, Wakili wa Serikali Faustine Sylvester amedai kuwa upande wa mashitaka uko tayari kwa ajili ya ushahidi.

“Upande wa mashitaka umekuja na shahidi mmoja ambapo tuko tayari kuendelea na kesi,”
Mara Dibogo akanyoosha mkono, Hakimu Lihamwike alimpa nafasi ya kuongea ambapo alidai kuwa anajisikia kizunguzungu toka atoke gerezani Segerea.

“Naumwa hali yangu sio nzuri toka nitoke Segerea lakini kwa kuwa kesi ilipangwa leo nimetii amri ya mahakama,” alidai Dibogo.
 

Hakimu Lihamwike alimhoji mshitakiwa wakati anasubiri kuitwa mahakamani alikuwa amekaa au amesimama alidai kuwa alikuwa amekaa.

Kabla ya Hakimu kuihairisha kesi hiyo Mshitakiwa huyo alianguka chini, Hakimu Lihamwike aliihairisha kesi hiyo hadi Desemba 11, mwaka huu kwa ajili ya kuendelea na ushahidi huo.

“Kesi na ihairisha hadi Desemba 11, mwaka huu haya amka uende,” alisema Hakimu.

Dibogo alidai kuwa hawezi kuamka na hakimu kuwataka askari kumsaidia mara mshitakiwa aliamka na kutoka nje huku akiwa anacheka.
 

Inadaiwa kuwa Dibogo alimbaka msichana wa miaka 14 na kumsababishia maumivu makali.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HADITHI:MWALIMU MAGDALENA sehemu ya 1

Hadithi: Mwalimu Magdalena sehemu ya 5

Hadithi: Mwalimu Magdalena sehemu ya 4