Mtu auwawa kwenye maandamano Mombasa

Waandamanaji walipora maduka na
kuwarushia mawe polisi kupinga kupigwa risasi na kuuwawa kwa mtu
anayeshukiwa kuwa mpiganaji Muislamu.
Polisi wanakanusha kuwa
walihusiuka na mauaji hayo yaliyotokea Jumamosi ya Hassan Guti, ambaye
alihusishwa na mauaji ya afisa mwandamizi wa polisi mwezi Agosti.
Inaarifiwa kuwa ghasia zilizuka Jumapili baada ya mazishi ya Bwana Guti.
Watu kadha wa msimamo mkali wa kidini wameuwawa mjini Mombasa katika miezi ya karibuni.
Kumetokea mashambulio kadha ya mabomu mjini humo, ambayo yanashukiwa kufanywa na kundi la wapiganaji Waislamu wa Somalia, Al Shabaab.-bbc
Maoni
Chapisha Maoni