Merkel : "Ndoto iliokuwa kweli " - Miaka 25 Kuanguka Ukuta wa Berlin

Kansela Angela Merkel Jumapili (09.11.2014) ameongoza sherehe za kuadhimisha miaka 25 ya kuanguka kwa Ukuta wa Berlin na kuuita huo kuwa mfano wa shauku ya binaadamu kwa uhuru. http://www.dw.de/image/0,,18050004_354,00.jpg
Kansela Angela Merkel akizungumza wakati wa ufunguzi wa maonyesho ya kuadhimisha miaka 25 ya kuanguka kwa Ukuta wa Berlin katika Kituo cha Kumbukumbu cha Bernauer Strasse. (09.11.2014)
Usiku wa Novemba 9 mwaka 1989 maelfu ya wananchi wa Berlin ya Mashariki walimiminika kwenye vituo vya mpakani ambavyo huko nyuma vilikuwa vimefungwa baada ya utawala wa kikomunisti kusalimu amri kutokana na shinikizo kubwa la umma na kukubali kuregeza vikwazo vya safari ambavyo vilikuwa vimewazuwiya raia wao kwenda Ujerumani magharibi kwa miongo kwa kadhaa.
"Kuanguka kwa Ukuta kumetuonyesha kwamba ndoto zinaweza kuwa za kweli". Merkel ametamka hayo katika eneo kuu la kumbukumbu ya Ukuta huo katika mtaa wa Bernauer Strasse mjini Berlin.
Kuanguka kwa Ukuta huo ilikuwa ni kilele cha wiki kadhaa za maandamano ya umma yaliyokuwa yamechochewa na mabadiliko ambayo yalikuwa tayari yametokea katika nchi nyengine za Ulaya mashariki.
Merkel ametaja mifano muhimu iliowekwa na makundi ya vuguvugu ya demokrasia nchini Poland,Czechchoslovakia na Hungary na kuwapongeza wananchi wa Ujerumani mashariki walioshajiishwa nao ambao walisimama kupambana na udikteta.-DW

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HADITHI:MWALIMU MAGDALENA sehemu ya 1

Hadithi: Mwalimu Magdalena sehemu ya 5

Hadithi: Mwalimu Magdalena sehemu ya 4