Maximo ampa mtihani Manji
KOCHA
Mkuu wa Yanga, Mbrazili Marcio Maximo, ameutaka uongozi wa klabu hiyo chini ya
Mwenyekiti Yusuf Manji kufanya kila wawezalo kuhakikisha wanamsajili kiungo
mahiri wa Mtibwa Sugar, Shaaban Nditi katika kipindi hiki cha dirisha dogo la
usajili lililofunguliwa juzi.
Nditi ni mmoja wa viungo wakabaji mahiri wachache hapa nchini, ambaye alishawahi kuwa chini ya Maximo wakati Mbrazil huyo akiinoa timu ya Taifa, Taifa Stars miaka ya 2006 hadi 2010.
Maximo yupo katika mikakati ya kukiimarisha kikosi chake, lakini nguvu zaidi akizipeleka katika kiungo mkabaji ili kumrejesha Mbuyu Twite katika nafasi ya beki wa kulia ambayo imeonekana kutoendana na kasi ya kikosi chake.
Taarifa za uhakika kutoka ndani ya Yanga zilizolifikia BINGWA jana, zinasema kuwa Nditi ndiye mchezaji anayetakiwa zaidi na Maximo, akiwamo Jonas Mkude wa Simba.
Kwa mujibu wa chanzo chetu cha uhakika, katika ripoti yake, Maximo amesema kuwa iwapo atampata Nditi au Mkude, atakuwa ametatua tatizo sugu linalomkabili na hivyo kukifanya kikosi chake kuwa tishio.
“Amependekeza jina la Nditi, kwani bado ana imani naye, pia alivutiwa jinsi alivyoonyesha kiwango kizuri katika mchezo tuliocheza na Mtibwa,” alisema.
Mtoa habari wetu huyo ambaye hakupenda kutajwa jina gazetini, alisema kuwa Maximo alisema Mtibwa walikuwa imara katika safu ya kiungo, chini ya Nditi hali iliyoisumbua mno Yanga na kushindwa kufurukuta.
Kuhusu Mkude, tayari kiungo huyo amesaini mkataba mpya wa miaka miwili zaidi kuitumikia Simba, ikiwa ni baada ya ule wa awali kutarajiwa kumalizika mwishoni mwa msimu huu.
Hata hivyo, katika kikosi cha Yanga kuna wachezaji mahiri wa safu ya kiungo wakabaji kama Omega Seme, Saluma Telela na Said Juma ambao wameshindwa kuaminiwa na Mbrazil huyo.

Maoni
Chapisha Maoni