Mauaji ya kutisha Bukoba
JESHI la Polisi mkoani Kagera linamshikilia, Issa Sadiki
(49) mkazi wa Itongo, Tarafa ya Nshamba, Wilaya ya Muleba, Kagera kwa tuhuma za
kuua watu watatu wa familia moja.
Mji wa Buoba

Issa anatuhumiwa kuwaua baba yake, Sadiki Hamis (84) kwa
kumtenganisha kichwa na kiwiliwili, mama yake mdogo Zamuda Sadiki (44) na mdogo
wake Juma Sadiki (15), aliyefariki akiwa katika Hospitali Teule ya Rubya
iliyopo Muleba.
Kamanda wa Polisi Mkoa
wa Kagera, Henry Mwaibambe, alisema tukio hilo lilitokea juzi saa mbili usiku
baada ya kundi la watu wasiojulikana kuvamia familia hiyo na kufanya unyama
huo.
Mwaibambe alisema watu hao walimwacha mtoto Aza Sadiki (19)
bila kumdhuru, ambaye ni mwanafunzi wa kidato cha tatu katika Shule ya Sekondari
Rukondo. Hata hivyo walimnyang’anya simu yake.

Alisema kulikuwa na ugomvi wa muda mrefu kwa madai kwamba
baba wa familia hiyo alikuwa akitoa huduma kwa upendeleo kwa mke wake wa nne
ambaye ni Zamuda.
“Kwa sababu Hamisi
alikuwa na wake wanne, yawezekana wake zake wengine watatu na watoto wao
walihisi kuna dalili ya mke mdogo kupewa nafasi kubwa ya kurithi mali pamoja na
mwanaye Juma aliyefia katika Hospitali ya Rubya,” alisema Kamanda Mwaibambe.
Aidha alisema chanzo cha tukio hilo ni urithi wa mali na
kuongeza kuwa Jeshi la Polisi linamshikilia Issa Sadiki kwa kuhusika na mauaji
hayo, na upelelezi unaendelea.-Chanzo MTANZANIA.
Maoni
Chapisha Maoni