Mashambulizi ya uhalifu yazusha wasi wasi wa usalama Kenya

Viongozi wa Kenya wamejitokeza Jumapili kulaani vikali mashambulizi
na mauwaji ya polisi 21 kaskazini mashariki ya Kenya na mashambulio
mawili katika kambi ya jeshi mjini Mombasa na kituo cha polisi mjini
Malindi.
Uhuru Kenyatta alitoa onyo kali kwa wafugaji wa County ya Turkana, alipotembelea mji wa Kapedo Jumapili mchana ambako maafisa hao wa polisi waliuliwa walipokuwa wanakwenda kutafuta gari moja la polisi la kupambana na ghasia lililowaka moto karibu na mji huo.
Rais Kenyatta alisema “mimi silaha hizo ambazo zilichukuliwakutoka hawa askar, mimi sitaki kungojea wiki mbili ninataka murudishe leo, lazima munajuwa wako wapi."
Kiongozi huyo wa Kenya aliwaonya pia wale watu wanaotaka kuwagawanya Wakenya kwa misingi ya kikabila.
“Kwa wale wanaofikiria watairudisha nchi hii nyuma kwa kutuletea siasa za karne zilizopita hizo hatuelewi sisi. TUnajuwa ya kwamba taifa hili ni la wananchi milioni 40 wa Kenya.”
Kwa upande wake naibu wake William Ruto, alihudhuria sala maalum katika kanisa la Holy Family Basilica, mjini Nairobi, sala iliyofanyika kwa ajili ya familia na marafiki wa maafisa walouliwa na hapo akawaonya pia wanaotaka kuleta vurugu nchini humo.
“Hakuna kundi, hakuna sehemu, hakuna gengi, litakalo washika mateka wakenya,, kwa kuchukua silaha na kujipanga na kupigana kuwauwa watumishi wetu wa usalama wakidhani wataachwa bila ya kufanywa lolote. Ninataka kuwaambia, wale wanaotaka kujaribu kupima aina gani ya chuma Kenya imetengenezwa nayo wenyeji au wageni, basi tunawaambia magaidi, washambuliaji mifugo, na wahalifu wote kwamba tutakusanya rasilmali zetu zote ili kuhakikisha tumewafikisha mbele ya sharia na watajibu kila kitendo walitokifanya.
Wakati Rais Kenyata anatembelea huko kaskazini mashariki ya nchi, maafisa wa usalama wa mji wa Mombasa waliripoti kutokea shambulizi lililofanywa katika kambi ya jeshi la Kenya, huko Nyali mjini Mombasa na watu walokua na visu, mapanga na miripuko.
Kamishna wa polisi wa County ya Mombasa, Nelson Marwa aliwambia waandishi habari kwamba huwenda washambulizi ni wanachama wa kundi lililopigwa marufuku la Mombasa republic council MRC kinachodai uhuru kutoka Kenya.
“Itakuwaje kundi la wahalifu wakiwa na akili zao wangelipanga kushambulia kambi ya jeshi katika nchi huru? Kwa hivyo katika shambulizi hilo watu sita waliuliwa kwa risasi na wengine kadha kukimbia wakiwa na majeraha.”
Hata hivyo gavana wa County ya Mombasa Ali Hassan Joho anachukulia mashambulio hayo kuwa ni vitendo vya uhalifu.
“Itakuwaje panakuwa na kundi dogo la watu wenye mapanga na visu wanajaribu kushambulia kambi ya kijeshi. Ndio, ni uhalifu mkubwa unaobidi kushughulikiwa, lakini hili suala la hivi sasa, kusema kambi huko Mombasa inashambuliwa, hilo kwa hakika sicho kinachotokea.
Kwa upande wake, Katibu mkuu wa MRC Randu Nzai Ruwa amekanusha katu kwamba kundi lake limehusika.
Na wakati shambulio la Nyali likitokea kulikuwa na shambulio jingine linatokea katika kituo kikuu cha polisi cha mji wa Malindi uliyopo kaskazini mwa Mombasa. Na naibu mkuu wa polisi wa mji huo, Kamanda Fredric Mwangi amesema kundi la watu 20 walokuwa na silaha walijaribu kushambulia kituo hicho cha polisi.
Maafisa wanawasaka walohusika na mashambulizi hayo ya malindi na Mombasa.-VoA

Maoni
Chapisha Maoni