Kiongozi wa dini auawa nchi Kenya

Masjid musa,mombasa
Watu wasiojulikani kwenye mji wa
pwani nchini Kenya ,Mombasa wamemuua kwa kumpiga risasi kiongozi
mashuhuri na mwenye msimamo wa wastani wa dini ya kislamu.
Sheikh
Salim Bakari Mwarangi ambaye ni mwanaharakati wa kampeni dhidi ya
itikadi kali alipigwa risasi wakati alipokuwa akirudi nyumbani kutoka
msikitini jumanne usiku.Viongozi sita wa dini ya kiislamu badhi yao wenye itikadi kali na wale walio na misimamo ya wastani wameuawa mjini Mombasa tangu mwaka 2012.
Eneo la pwani ya kenya lenye waislamu wengi limekumbwa na misururu ya mashambuli ya mabomu yanoyoaminika kutekelezwa na watu walio na uhusiano na kundi la Al shabaab lenye makao yake nchini Somalia.-BBC swahili
Maoni
Chapisha Maoni