Kiongera aanza mdogomdogo

MSHAMBULIAJI wa Simba Mkenya Raphael Kiongera amepanga kuanza
mazoezi ya gym leo Jumatatu lakini ametamka neno moja tu kwamba atarudi
uwanjani kuongeza nguvu ya ushindi katika kikosi chake cha Simba.
Kiongera aliumia goti wakati wa mechi ya kwanza ya
Ligi Kuu Bara dhidi ya Coastal Union na kulazimika kukaa nje ya uwanja
kwa wiki nane ambayo ni sawa na miezi miwili na sasa anaendelea vizuri
ingawa amesema matokeo wanayopata sasa hayamfurahishi.
Kiongera aliwataka wachezaji wa Simba kutokata
tamaa na matokeo hayo bali wanahitajika kupambana zaidi na kuona mwisho
wao ni upi kwa kile alichoeleza kuwa katika soka lolote linaweza
kutokea, ni kufungwa, kushinda na sare.
“Jumatatu nitaanza mazoezi ya gym ila sijajua
nitafanya kwa muda gani, goti langu linaendelea vizuri kwani hata yale
maumivu siyasikii kwa sasa, natamani kucheza ili nisaidiane na wenzangu
kuhakikisha tunaitoa Simba hapa ilipo, naamini nikipona nitaungana nao.
“Matokeo haya siyo mazuri kwetu na yanasikitisha
na kukatisha tamaa, hivyo ni lazima kutafuta sababu ya nini kinafanya
matokeo haya yatokee hivi mfululizo ingawa soka ni mchezo wa makosa, ila
tukipambana naamini tutafanya vizuri mechi zijazo,” alisema Kiongera.-mwanasport
Maoni
Chapisha Maoni