Kala kuizindua Usikate Tamaa

Mkali wa muziki wa Hip Hop nchini, Kala Jeremiah Masanja anatarajiwa
kuzindua video ya wimbo wake mpya utakaokwenda kwa jina la ‘Usikate Tamaa’,
utakaofanyika Jumapili hii kwende Ukumbi wa New maisha Club.
Kala amesema audio na video ya wimbo huo aliomshirikisha
msanii Nuruwell, vitasikika na kuonekana kwa mara ya kwanza siku hiyo kwa
mashabiki watakaohudhulia kwenye uzinduzi huo.
Amesema uzinduzi huo pia utasindikizwa na wasanii Mo Music, Stamina,
Ben Pol, Ney Lee pamoja na Nuruwell.
“Mashabiki watakaofika siku hiyo ndiyo watakaokuwa wa kwanza
kuusikia na kuuona wimbo huo ambao ndio utakuwa unazinduliwa rasmi."
Maoni
Chapisha Maoni