Jeshi la Burkinafaso litaunda serikali ya umoja wa kitaifa.

Luteni Kanali  Yacouba Isaac Zida (L) akutana na kiongozi wa upinzani katika mji mkuu wa  Burkina Faso, Ouagadougou,Nov. 2, 2014.

Jeshi la Burkinafaso ambalo lilichukua madaraka Ijumaa, limetangaza kwamba litaunda serikali ya umoja wa kitaifa ili kusimamia kipindi cha mpito kilichosababishwa na kuondolewa kwa rais wa muda mrefu Blaise Compaore .
Taarifa fupi iliyotolewa jana usiku imeeleza kwamna kila kitu cha serikali ya mpito kitaidhinishwa kwa maridhiano  ya pamoja lakini haikutoa maelezo ya jinsi gani itafanyika.
Tangazo la Jumapili huko Ouagadougou limefuatia saa kadhaa  za mkanganyiko wa nani ataongoza taifa hilo maskini la watu milioni 17.
Muda mfupi baada ya kujiuzulu Bw.Compaore kwa lazima, wakuu wawili wa jeshi walijitokeza ni kila mmoja alidai kuwa  ni kiongozi mpya. Na hapo tena Jumamosi, jeshi lilimtaja mmoja wao Luteni kanali Yakuba Isaac Zida kuwa ataiongoza serikali ya mpito, lakini upinzani umepinga.-VoA
 
Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HADITHI:MWALIMU MAGDALENA sehemu ya 1

Hadithi: Mwalimu Magdalena sehemu ya 5

Hadithi: Mwalimu Magdalena sehemu ya 4