Genge lakiri kuwaua wanafunzi 40 Mexico

Mkuu wa sheria nchini Mexico
anasema kuwa genge moja la wahalifu limekiri kuwaua zaidi ya wanafunzi
40 ambao walitoweka wiki kadha zilizopita.
Jesus Murillo alisema
kuwa wanachama wa genge la madawa ya kulevya la Guerreros Unidos
linasema kuwa liliwaua wanafunzi hao na kisha likachoma maiti zao.Kundi hilo lilisema kuwa lilikabidhiwa wanafunzi hao na polisi baada ya makabiliano kwenye mji wa Iguala.
Mkuu huyo wa sheria anasema kuwa mabaki ya maiti hizo yamepatikana kando ya mto na uchuguzi wa DNA utafanyika nchini Austria ili kuitambua.
Familia za wanafunzi hao zinasema kuwa zinaamini kuwa wanafunzi hao bado wako hai.
Meya wa mji wa Iguala yuko kizuizini kufuatia kuwaamrisha polisi kuingilia kati ili kuwazuia wanafunzi hao kuandamana.-BBCSWAHILI
Maoni
Chapisha Maoni