Coutinho atuma ujumbe mzito
KIUNGO
mshambuliaji wa Yanga,
Mbrazil Andrey Coutinho
ambaye kwa sasa yupo nchini kwao kwa mapumziko mafupi baada ya kusimama kwa
Ligi Kuu Tanzania Bara, amewataka mabeki wa timu watakazokutana nazo kujiandaa
kuchuana naye akiwa katika mwonekano tofauti na ule wa awali.

Mbrazil huyo amesema kuwa baada
ya kuwapo hapa nchini kwa takribani miezi minne, kuna jambo kubwa alilojifunza
ambalo anaamini akilifanyia kazi huko, mashabiki wa Yanga watafurahi kwani
amebaini wachezaji wa Tanzania wanatumia nguvu nyingi zaidi hivyo ili kupambana
nao, kunahitajika nguvu za kutosha.
Ni kutokana na hilo, tangu ametua
Brazil, amekuwa akijifua vilivyo kusaka stamina, akihudhuria mazoezi hayo ya
viungo katika klabu mbalimbali za mazoezi (gym), lakini pia akikimbia katika
maeneo mbalimbali, ikiwamo ufukweni.
Coutinho mwenye uwezo mkubwa wa
kumiliki mpira na kupiga adhabu, kona na krosi za nguvu kwa kutumia mguu wa
kushoto, amesema kuwa anataka kurejea nchini kivingine na hivyo kufanya kweli
kwenye mechi zao zijazo ili kuwafurahisha mashabiki wa Yanga.
Alisema kuwa anafahamu mechi yao
ijayo itakuwa dhidi ya Simba katika mchezo wa Nani Mtani Jembe ambapo
anatarajia kuanza kuonyesha cheche zake siku hiyo akiwa katika sura mpya.
Mchezo huo wa Nani Mtani Jembe
unatarajiwa kupigwa Desemba 12, mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.-Chanzo Gazeti la bingwa
Maoni
Chapisha Maoni