Auwawa kwa kupigwa Risasi

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiPBn1hrJg8Ogd333w08Hq2bl6WMsvSCEGrpS9796LXC4RnsGxS1q0iy1tWNn509oEu1qH3YKUHECvGV1rBOFAZ2MpmRCvIR0TVXU9-sBlW8QFTT71nuMrhXu7F32VkGopnyEJX-XhqthkT/s640/CIMG5238.JPGMTU mmoja  John     Salehe (32) Mkazi wa Kijiji  cha  Itenka  Wilaya ya Mlele mkoani  hapa,  ameuwawa kikatili  kwa  kupigwa  risasi  kichwani  na kifuani  na mtu asiye julikana  wakati akinywa pombe baani
Akizungumza na waandishi wa habari jana, Kamanda Polisi Mkoa wa Katavi,Dhahiri Kidavashari alisema  tukio hilo  lilitokea juzi saa mbili usiku.
Alisema kabla ya  tukio  hilo, marehemu alikuwa  kinywa pombe  katika baa inayomilikiwa  na Mussa Juma.
Alisema mtu asiyefahamika alifika hapo  na kufyatua risasi mbili  zilizompiga  marehemu  kifuani  na kichwani.
Alisema katika tukio hilo,James  Omar(30) mkazi wa kijij cha Itenka  alijeruhiwa  kwa kupigwa  na risasi eneo la kiunoni.
Alisema majirani  wa eneo  hilo, walifika eneo hilo kwa lengo la kutow msaada hata hivyo  walikuta  muhusika aliyafanya tukio hilo, ametoweka.
               
Chanzo  cha  tukio  hilo bado  halijajulikana  na hakuna mtu aliyekamatwa.
Kamanda Kidavashari,alisema polisi wanaendelea na msako  dhidi ya watu waliohusika.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HADITHI:MWALIMU MAGDALENA sehemu ya 1

Hadithi: Mwalimu Magdalena sehemu ya 5

Hadithi: Mwalimu Magdalena sehemu ya 4