Ukatili wa polisi marekeni dhidi ya watu weusi waendelea

Vitendo vya ukatili na ukandamizaji
wa polisi dhidi ya raia wa Marekani wenye asili ya Kiafrika vingali
vinaendelea. Jana kulisambazwa video mpya ya ukatili wa polisi dhidi ya
kijana mwengine mwenye asili ya Kiafrika huko New York, Marekani, ambayo
inamuonyesha kijana huyo akipigwa vikali na kutukanwa na polisi na
kisha kukandamizwa ardhini.
Kwa mujibu wa video hiyo, kijana huyo
anayefahamika kwa jina la Hamer na anayedhaniwa kuwa na umri wa miaka
17, alishambuliwa na polisi kwa kisingizio cha kuvuta bangi. Habari
zinasema kuwa, licha ya kijana huyo kufanyiwa ukatili huo bila ya kuwa
na utetezi wowote na yeye kuishia kupiga kelele za kuomba msaada, lakini
alikutwa akivuta sigara ya kawaida tu kinyume na madai ya polisi kuwa
alikuwa akivuta bangi.
Wazazi wa kijana huyo wamesema kuwa kijana wao
amepata matatizo katika ubongo wake kutokana na kipigo kikali
alichokipata kiasi kwamba hawezi tena kufanya kazi yoyote yeye mwenyewe
bila ya msaada. Hii ni katika hali ambayo hivi karibuni pia,
kulisambazwa video iliyomuonyesha polisi wa Marekani wakimuadhibu vikali
raia mwengine mwenye asili ya Kiafrika kwa kosa la eti kuendesha gari
bila kuvaa mkanda.-Iran
Maoni
Chapisha Maoni