Yanga yashusha mastaa Kagame,yamzuga Kiiza
Lakini watani wa Yanga baada ya kusikia uamuzi wa
Maximo wakaanza kukejeli kwamba amekimbia lawama ingawa yeye ameeleza
wazi programu yake.
Wakati Neiva na Nsajigwa wakienda kupambana nchini
Rwanda Maximo ataungana na kocha wa kikosi cha timu ya vijana ya klabu
hiyo, Salvatory Edward kuweka kambi Pemba.
Yanga imepangwa kundi A katika michuano hiyo na
itatupa karata yake ya kwanza Agosti 8 dhidi ya Rayon Sports ya Rwanda.
Japo Maximo amefanya siri juu ya kikosi kitakachokwenda kwenye kombe la
Kagame, Mwanaspoti linafahamu kuwa wachezaji walioko na timu za taifa
ni Oscar Joshua na Nadir Haroub Cannavaro pekee watakaoungana na kikosi
hicho.
Oscar anapewa nafasi kubwa ya kwenda kutokana na
nafasi anayoicheza kuwa na mchezaji mmoja tu Amosi Abel kutoka timu ya
vijana huku Cannavaro akienda kutokana na kukosekana kwa beki mzoefu wa
kati.
Mwanaspoti linafahamu kuwa Katika wachezaji
waliofanya mazoezi na Maximo tangu mwanzo watakaoenda Rwanda kwenye
michuano hiyo ya Kagame kwa mujibu wa mazoezi ni makipa Juma Kaseja,
Ally Mustapha ‘Barthez’ na Said Ally wa timu ya vijana.
Mabeki watakaoongozana na kikosi hicho ni Juma
Abdul, Said Juma, Rajab Zahir, Salum Telela, Issa Ngao, Amosi Abel,
Oscar na Cannavaro. Viungo ni Mbuyu Twite na Omega Seme (kama viungo
wakabaji) , Hassan Dilunga na Hamis Thabiti kama viungo washambuliaji.
Wabrazil Andrey Coutinho na Genilson Santos ‘Jaja’, Saidi Bahanuzi na
Jerry Tegete ndio wakataoongoza safu ya ushambuliaji.
Wachezaji wengine watakaokwenda na kikosi hicho ni
Nizar Khalifan na Hussein Javu ili kukamilisha idadi hiyo ya wachezaji
21. Maximo alisema, “Mimi sitakwenda na timu, watakwenda Nsajigwa
(Shadrack) na Leonardo (Neiva) na kikosi cha wachezaji kati ya 20 ama 21
pekee, kati ya hao mmoja au wawili pekee anayetoka kwenye majukumu ya
kitaifa ndiyo watakaojiunga na timu.
“Mimi na Salvatory (Edward) tutasafiri na
wachezaji wengine wanaotoka kwenye timu za Taifa pamoja na hawa
wanaobaki kwenda Pemba (visiwani) kuweka kambi, tutafanya mazoezi mpaka
watakaporejea kutoka Kagame.”
“Watakaokwenda na timu Kagame wataandika ripoti na
pia nitazitazama picha za video, baada ya hapo tutafanya tathmini na
kupanga kikosi imara kwaajili ya mapambano,” alisema Maximo huku katika
mazoezi ya jana wachezaji wa Yanga akiwemo Coutinho na Juma Abdul
wakimchezesha Jaja kiutamu tofauti na siku za nyuma.
Maoni
Chapisha Maoni