Watoto wazidi kutumiwa vitani Sudan

HRW: Watoto wazidi kutumiwa vitani Sudan Kusini
Shirika la kutetea haki za binadamu la Human Rights Watch (HRW) limesema kuwa, idadi ya watoto wanaotumikishwa vitani nchini Sudan Kusini imeongezeka kufuatia mapigano yanayoendelea kati ya vikosi vya jeshi la serikali na waasi.
Mkurugenzi Mtendaji wa HRW barani Afrika Daniel Bekele amesema kwamba, jeshi la Sudan Kusini limeanza tena hatua zisizofaa za kuwatumikisha vitani watoto na kwamba raia na viongozi wa kijeshi wanapaswa kuwaondoa watoto vitani na kuwarejesha katika familia zao haraka iwezekanavyo.
Kwa mujibu wa Human Rights Watch waasi pia wanawatumisha kwa lazima watoto vitani.
Kuanzia mwezi Disemba mwaka jana, Sudan Kusini ilitumbukia katika machafuko baada ya kuzuka mapigano kati ya askari watiifu kwa Rais Salva Kiir wa nchi hiyo na makamu wake wa zamani Riek Machar katika mji mkuu Juba. Mgogoro huo uligeuka vita vya ndani na kusababisha vifo vya watu wengi huku wengine wakilazimika kuwa wakimbizi.-Crdt iran swahili

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HADITHI:MWALIMU MAGDALENA sehemu ya 1

Hadithi: Mwalimu Magdalena sehemu ya 5

Hadithi: Mwalimu Magdalena sehemu ya 4