Wapiganaji wa Kurdi washikilia Monsul

wapiganaji wa Kikurdi
Wapiganaji wa Ki Kurdi waliopo kaskazini mwa iraq
wamesema kuwa kwa sasa wanadhibiti eneo lote la bwawa la Mosul baada ya
kulikomboa kutoka kwa wapiganaji wa Kiislam kwa mapigano ya siku mbili
mfululizo.
Mwandishi wa BBC aliyepo katika bwawa hilo
anasema amesikia milio ya risasi na milipuko eneo karibu kabisa na
Wakurdi ambapo jeshi la Iraq linaendelea kuklabiliana na wapiganaji hao
wa Kiislam ili kuwaondoa katika eneo hilo.Hata hivyo kusini mwa Iraqi pia majeshi ya serikali yameendelea kupambana na makundi ya wapiganaji wa Kishia ili kuukomboa mji wa Tikrit unaokaliwa na wapiganaji hao japo kuwa inadaiwa kuwa wanakabiliwa na upinzani mkali..
Maoni
Chapisha Maoni