Tetemeko la ardhi latikisa Afrika Kusini

Tetemeko la ardhi limetokea
Afrika Kusini na kumuua mtu mmoja pamoja na kusababisha wachimba migodi
kukwama katika machimbo Kusini Magharibi mwa Johannesburg.
Waokozi wanasema kuwa tetemeko hilo lilikuwa
lenye vipimo vya 5.3 na lilitokea katika eneo la Orkney, kitovu cha
machimbo ya dhahabu.Maafisa wa uokozi walisema kwamba shughuli ya uokozi ilitakiwa kufanyika katika migodi inayozingira Orkney ingawa moja ya mgodi ulikuwa na tatizo.
Mwandishi wa BBC mjini Johannesburg anasema kuwa eneo linalozingira mji huo, lina historia ya kukumbwa na mitetemo ya ardhi katika migodi ingawa yenye vipimo vya chini.
Migodi hiyo ya dhahabu ni ya kina kirefu
Wanajiolojia wametaja tetemeko hilo kama lenye kuonyesha dalili muhimu kwani lilitetemesha madirisha katika majengo marefu mjini Johannesburg.-BBC
Maoni
Chapisha Maoni