Sudani waomba muafaka

Marais wa Sudan Mbili wataka kutatuliwa matatizo
Marais wa Sudan na Sudan Kusini wamesisitiza juu ya azma ya nchi zao ya kupatiwa ufumbuzi matatizo yaliyopo kati ya nchi hizo mbili. Marais Omar Hassan al-Bashir na Salva Kiir wamesisitiza hayo katika mazungumzo yao waliyoyafanya kwa njia ya simu na kueleza kwamba, wanataka matatizo yaliyopo kati ya Juba na Khartoum yapatiwe ufumbuzi. Rais Omar al-Bashir amesisitiza katika mazungumzo hayo kwamba, Khartoum inataka amani na uthabiti upatikane katika nchi jirani ya Sudan Kusini. Wakati huo huo, Abdul Rahman Muhammad Hussein, Waziri wa Ulinzi wa Sudan ametoa wito wa kuharakishwa utekelezwaji wa makubaliano ya usalama yaliyotiwa saini kati ya Khartoum na Juba Disemba mwaka 2012 huko Addis Ababa, Ethiopia. Tangu Sudan Kusini ilipojitenga na Sudan na kujitangazia uhuru wake Julai 9 mwaka 2011 imekuwa ikivutana na jirani yake huyo kuhusiana na masuala mbalimbali likiwemo la mipaka-Chanzo iran swahili

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HADITHI:MWALIMU MAGDALENA sehemu ya 1

Hadithi: Mwalimu Magdalena sehemu ya 5

Hadithi: Mwalimu Magdalena sehemu ya 4