S.Leone yapiga marufuku Kandanda

Mechi za soka zapigwa marufuku nchini Sierra Leone.
Shirikisho la soka la Sierra
Leone limepiga marufuku mechi zote za kandanda nchini humo ikihofia
kuenea zaidi kwa maradhi ya homa ya Ebola.
Hatua hiyo inafuatia marufuku iliyotangazwa na
rais Ernest Bai Koroma katika jitihada za kuzuia kuenea zaidi kwa
maradhi ya ebola nchini humo.Hali hiyo ya tahadhari iliyotangazwa na rais inatarajiwa kudumu kwa kipindi cha siku 60 hadi 90.

S.Leone ilikuwa inatarajiwa kuikaribisha Cameroon mwezi ujao
Kufuatia marufuku hiyo huenda taifa hilo
likakosa kuandaa mechi ya kufuzu kwa dimba hilo dhidi ya timu ya taifa
na Cameroon iliyokuwa imeratibiwa kuchezwa mwezi ujao.Aidha maandalizi ya mechi ya ufunguzi ya kundi D dhidi ya Ivory Coast inatarajiwa pia kuathirika.
Marufuku hiyo pia itaathiri pakubwa maandalizi na mechi za mkondo wa pili wa ligi ya Sierra Leone.
Timu ya Sierra Leone imekuwa nchini Kenya kwa zaidi ya juma moja baada ya maafisa wa usalama wa uma wa kisiwa cha Ushelisheli kuwanyima ruhusa ya kuingia huko kufuatia hofu wanaweza kuleta maambukizi ya ugonjwa huo.
Makataa hiyo iliifaidi timu ya Sierra Leone ambayo ilijizolea alama tatu bila hata kutoa kijasho.-BBC swahili
Maoni
Chapisha Maoni