Pluijm, Mkwasa wachemka Saudi Arabia

MAKOCHA
wa zamani wa Yanga, Mholanzi Hans Van Der Pluijm na Boniface Mkwasa,
wamekatisha mikataba yao na klabu ya Al Shoalah FC ya Ligi Kuu Saudi
Arabia baada ya klabu hiyo kuwalazimisha kwa kuwasajilia wachezaji
wasiokuwa na viwango huku matatizo ya kifedha na kiongozi yakiathiri
maendeleo ya uwanjani.
Pluijm alisema: “Kwa bahati mbaya mambo hayakuenda
vizuri. Ni kinyume na tulivyotarajia. Mimi na kocha Mkwasa,
tumefundisha klabu hiyo kwa takribani wiki tatu na sasa tumeamua
kuachana nayo kwa sababu ya matatizo ya uongozi na kifedha yanayoikumba
klabu hiyo.Matatizo hayo yalikuwepo toka mwanzoni tulivyowasili kwenye
hiyo klabu.”
Pluijm pia alisema kuwa walikuwa na mahusiano na wakati mzuri na wachezaji na kwamba walikuwa na furaha kwa kupata mafunzo yao.
“Wachezaji walikuwa wakituamini na kupenda jinsi
tulivyokuwa tukiwafundisha, walikuwa wakitueleza kuwa wanaona mambo
yamebadilika tangu tulipowasili,” alisema.
Naye Mkwasa aliyekuwa Kocha Msaidizi alisema:
“Walituletea wachezaji wa ligi daraja la tatu ili tuwatumie kwa ajili ya
ligi kuu. Wachezaji hao hawakuwa na viwango na hivyo viongozi wa timu
walidai kutoridhika na ushirikiano wetu kwao na wakalazimu kuvunja
mikataba yetu.
“Sisi ni makocha wa kimataifa, hatufanyi kazi kwa kubabaisha.”-MWANASPORT
Maoni
Chapisha Maoni