Obama awataka viongozi Iraq waungane

Obama awataka viongozi Iraq waungane ilikupambana na Islamic State
Rais wa Marekani Barack Obama
ameonya kuwa hakuna njia rahisi ya kuisaidia serikali dhaifu ya Iraq
kukabiliana na wapiganaji wa kiislamu wa Islamic State.
''Itachukua muda mrefu kwa majeshi yetu kuisidia
Iraq kuwashinda wapiganaji wa Kisunni ambao wametangaza himaya yao
inayojumuisha ardhi katika mataifa ya Iraq na Syria ''Alisema Obama
Majeshi ya Marekani yashambulia Wapiganaji Islamic State
Obama alisema kuwa itawabidi viongozi wa Iraq kuungana ilikupambana na Islamic State.Rais Obama aliruhusu majeshi yake kuishambulia ngome ya Islamic State Ijumaa kwa mara ya kwanza ambapo majeshi ya Marekani imehusika katika vita moja kwa moja nchini Iraq tangu mwaka wa 2011.

Wakimbizi kutoka jamii ya Yazidi wakitorokea maisha yao
Mashambulizi hayo dhidi ya wapiganaji wa IS
iliharibu uwezo wao wa kuwashambulia jamii ya Yazidi ambayo ilikuwa
imetorokea milima ya Sinjar baada ya Islamic State kuteka mji wa
Qaraqosh.Mapema leo ndege za kijeshi za Uingereza zimefunga safari kusaidia utoaji wa misaada ya kibinadamu nchini Iraq.- BBC SWAHILI
Maoni
Chapisha Maoni