Obama awaaga marais wa Afrika Marekani


Siku tatu za mazungumzo yaliyolenga mustakabali wa bara la Afrika yamemalizika mjini Washington Marekani.
Mkutano huo ulikuwa wa kwanza wa aina yake kati ya Marekani na viongozi wa Afrika na ulilenga kuimarisha uhusiano kati ya Marekani na bara la Afrika.
Marais 40 wa Afrika walikwenda Marekani kuona kile ambacho Rais Obama alikuwa amewaitia katika jitihada zake za kuimarisha uhusiano kati ya Marekani na Afrika.
Waliondoka nchini humo wakiwa na mikataba ya uwekezaji ambapo makampuni ya Marekani yameahidi kuwekeza katika nchi za afrika.
Mikataba hiyo ni ya thamani ya dola bilioni 14 pamoja na ahadi ya Marekani kuimarisha uchumi na mataifa ya Afrika pamoja na mchango mwingine wa pesa ili kuimrisha miundo mbinu na upatikanaji wa kuwin barani humo.
Swala la usalama na ulinzi pia limeangaziwa
Marekani sasa imejitolea kuunga mkono kikosi cha dharura cha Muungano wa Afrika pia itatoa vifaa zaidi na walinda amani nchini Somalia na katika Jamhuri ya Afrika ya Kati.
Viongozi wa Afrika wanafahamu kuwa Marekani inashindana na China na mataifa mengine yaliyostawi kwa sababu tu kutaka kuwa na ushahwishi mkubwa Afrika.
Lakini hakuna Rais anayeweza kukosa kukubali msaada kutoka kwa nchi tajiri zaidi duniani kwa hilo.
Rais Obama amesema kuwa mazungumzo aliyofanya na marais wa Afrika yalikuwa ya kweli na yalitoa fursa ya kuweza kusikilizana na kuelewana.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HADITHI:MWALIMU MAGDALENA sehemu ya 1

Hadithi: Mwalimu Magdalena sehemu ya 5

Hadithi: Mwalimu Magdalena sehemu ya 4