Netanyahu:Usalama wa Israel uzingatiwe

Benjamin Natenyahu
Waziri mkuu nchini Israel Benjamin Netanyahu amesema
kuwa hakutakuwa na makubaliano ya kusitishwa vita kwa mda mrefu hadi
pale mahitaji ya usalama wa Israel yatakapozingatiwa.
Wajumbe wanaowakilisha Israel na Palestina
wanakutana katika mji mkuu wa Cairo nchini Misri ili kuendelea na
mazungumzo yao yasio ya moja kwa moja kutafuta mwafaka wa kusitisha vita
katika eneo la Gaza.Netanyahu ameliambia baraza la mawaziri kwamba ujumbe wa Israel katika mazungumzo hayo una jukumu la kuwa na msimamo mkali kuhusu mahitaji hayo ya kiusalama.
Kundi la wapiganaji wa Hamas linataka Israel na Misri kuondoa vikwazo vya mipakani dhidi ya Gaza huku Israel ikilitaka kundi la Hamas kusalimu silaha zao.-bbc
Maoni
Chapisha Maoni