Mwanamke auwawa kwa kuchunywa ngozi Mbeya


WATU wasiofahamika wamemuua mkazi wa kijijicha Idiwili, Kata ya Iyuli wilayani Mbozi na kumchuna ngozi ya shingo.
Pamoja na kumchuna ngozi marehemu ,wauaji hao pia walinyofoa macho ,ulimi na koromeo la marehemu
Baada ya mauaji hayo ya kinyama wauaji hao waliutelekeza porini mwili wa marehemu huyo Angelina Kameza mwenye umri wa miaka 26
Kaimu kamamda wa wa Polisi Mkoa wa Mbeya ,Barakaeli Maski alisema
"Tumepokea taarifa ya mauaji hayo ya kinyama lakini bado tunaendelea na upelelezi kujiua chanzo chake ni kipi, hatuwezi kuhusisha tukio hili na imani za ushirirkina kama baadhi wanvyo sikika ila uchunguzi unafanyika kwakuwa mwili wa marehemu ulikutwa ukiwa hauna baadhi ya viungo,
"Lakini uchunguzi wa awali unaonyesha marehemu alikuwa katika ndoa ya wanawake sita baada ya kuolewa na mwanaume mwenye umri wa miaka 70 aliye zaa nae watotot wawili,kabla ya kuolewa na mzee huyo, enzi za uhai wake aliolewa na mwanuaume mwingine katika mazingira yanayofanana  na haya kwani naye alinyofolewa baadhi ya viungo vya mwili  vikiwemo macho,ulimi na koromeo"alisema kamanda Msaki
Aliwataka wananchi kutoa taarifa katika vyombo vya dola watakapo pata taarifa za wauaji hao.-gazeti MTANZANIA AUG 18

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HADITHI:MWALIMU MAGDALENA sehemu ya 1

Hadithi: Mwalimu Magdalena sehemu ya 5

Hadithi: Mwalimu Magdalena sehemu ya 4