Marekani yashindwa kukomboa raia wake Syria

Matamshi hayo yametolewa na maafisa wa Marekani siku moja baada ya kundi la ISIL kutoa video inayoonesha mwandishi habari James Foley akikatwa kichwa. Hata hivyo Rais Barack Obama amesema kuwa, Marekani itaendelea kufanya kila iwezalo kuwalinda raia wake akidai kwamba kukatwa kichwa mwanahabari huyo kumethibitisha kuwa kundi la Daesh halina dini.
Ikumbukwe kuwa kundi hilo la kigaidi na mengine yanayopigana nchini Syria kwa karibu miaka mitatu sasa dhidi ya serikali ya nchi hiyo yamekuwa yakisaidiwa kwa hali na mali na nchi za Magharibi hususan Marekani na waitifaki wake wa Mashariki ya Kati kama Saudi Arabia an Qatar.-chanzo iran swahili
Maoni
Chapisha Maoni