Marekani yashambulia Wanamgambo wa IS

Ndege za Marekani zilizotekeleza mashambulizi dhidi ya IS
Wizara ya ulinzi nchini Marekani
inasema kuwa ndege za jeshi la Marekani zimefanya mashambulizi ya
angani dhidi wanamgambo wa kundi la Islamic state kaskazini mwa Iraq.
Pentagon ilisema kuwa ndege zilishambulia vituo
vilivyokuwa vikitumiwa kushambulia vikosi vya kikurdi vinavyopigana
kulinda ngome ya mji wa mji wa Irbil.Siku ya Alhamisi rais wa marekani Barack Obama aliamrisha kufanyika kwa mashambulizi ya angani dhidi ya wanamgambo wa kisuni ambao wameteka kiasi kikubwa cha ardhi ndani ya Iraq na pia ndani ya Syria.

Jamii ya Yazidi inayolengwa na IS
Rais Obama alisema kuwa wapiganaji wa kundi la
Islamic State watalengwa iwapo wataelekea kwenye mji wa kikurdi wa Irbil
au kwa lengo la kuzuia kile alichokitaja kama vitendo vya mauaji ya
halaiki dhidi ya wakristo na jamii za Yazidi.Hatua ya Marekani inajiri kukiwa na wasiwasi mkubwa wa uwezo wa wanamgambo hao kuteka sehemu kubwa zaidi ya Kaskazini mwa Iraq mbali na sehemu kubwa ya Syria.
Rais Obama amewashutmu wanamgambo wa Islamic State kwa kujaribu kuiangamiza jamii nzima na ya Yazidi akisema kuwa serikali yake itachukua hatua za kuzuia kutokea kwa mauaji ya halaiki.

Wapiganaji wa Kikurdi wanaokabiliana na IS
Ndege za jeshi la marekani zimekuwa zikiangusha
misaada huku nayo Uingereza ikisema kuwa itajiunga kwenye jitihada za
kutoa misada.Kiongozi wa dhebu la shia nchini Iraq Ayatollah Ali al Sistani amewataka wanasiasa nchini Iraq kungana na kumaliza ghasia huku naye kiongozi wa kanisa katoliki duniani papa Francis akisema kuwa atatuma mmoja wa viongozi wa kanisa hilo kama njia ya kuonyesha umoja .
Mnamo mwezi juni IS, awali ikijulikana kama Isis, iliteka mji wa Mosul kisha kundi hilo likauteka mji wa wenye wakristu wengi Qaraqosh

Wakimbizi wa ndani kwa ndani Iraq
Kulingana na Idara ya usalama ya Marekani
Pentagon ndege mbili za F/A-18 zilidondosha mabomu yenye paundi 500
ilikukaharibu ngome ya mashambulizi ya IS inayotumika kuishambulia mji
wa Irbil.Mji huo wa Irbil ni mwenyeji wa kikosi cha wanajeshi wa Marekani.
Hii ndiyo mara ya kwanza kwa jeshi la Marekani kujihusisha katika mapigano ndani ya Iraq tangu mwaka wa 2011.
Waziri wa maswala ya kigeni wa Marekani John Kerry ameonya jamii ya kimataifa kugutuka na kutahadhari dhidi ya ufanisi wa kundi hilo la wanamgambo wa IS.- Chanzo BBC SWAHILI
Maoni
Chapisha Maoni