Maiti ya albino yatupwa kwenye dimbwi la maji dar

 


Maiti ya albino anaekadiliwa kuwa na umri kati ya miaka 25 hadi 30 imekutwa ikielea katika dimbwi la maji eneo la tabata Kinyerezi  Mtaa wa Kanga Dar es salaam.
Habari zinasema watoto walio kuwa wakikata miwa katika eneo hilo ndiyo walio ikuta maiti hiyo ikiwa imetobolewa macho na wakapiga kelele za kuombas msaada .
Kamanda wa Polisi mkoa wa polisi wa Ilala, Mary Nzuki anasema mtu huyo alionekana juzi saa 11 jioni akiwa anaelea kwenye dimbwi la maji.
kamanda Nzuki aliongeza kuwa Marehemu alikuwa amevaa suruali ya kaki,viatu vya kike huku akiwa na majeraha usoni,kiunoni,machoni,kifuani na mdomo ukiwa umepinda.-LIMERIPOTI GAZETI LA MTANZANIA- AUG 18

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HADITHI:MWALIMU MAGDALENA sehemu ya 1

Hadithi: Mwalimu Magdalena sehemu ya 5

Hadithi: Mwalimu Magdalena sehemu ya 4