Juba haina nia ya kukomesha machafuko

Kiongozi wa waasi wa Sudan Kusini ameituhumu serikali ya nchi hiyo kwamba haina nia ya kweli ya kukomesha mgogoro kwa njia ya mazungumzo.
Riek Machar ametoa tarifa akisema kuwa serikali ya Juba inafadhilisha kununua silaha nzito na kuendelea kuua raia. Machar pia amekanusha madai yaliyotolewa na seikali ya Sudan Kusini kwamba kundi lake limepewa misaada ya silaha kutoka Sudan na kusisitiza kuwa silaha zinazotumiwa na wapiganaji wake zilichukuliwa ngawira kutoka kwa vikosi vya jeshi la serikali. Ameitaka serikali ya Juba kutupilia mbali masharti yake na kudumisha mazungumzo ya kusaka amani. Riek Machar pia amesema anasikitishwa na hatua ya serikali ya Juba ya kujiondoa katika mazungumzo ya Addis Ababa.
Jumamosi iliyopita wawakilishi wa serikali ya Sudan Kusini hawakuhudhuria kikao cha upatanishi kwa ajili ya kuunda kamati za masuala ya usalama, uchumi na serikali ya mpito.-Chanzo Iran swahili
Maoni
Chapisha Maoni