JESHI LA POLISI KUTUMIA TEKNOLOJIA KUPAMBANA NA UHALIFU

JESHI la polisi nchini limejipanga kufanya kazi zake kisasa kwa kutumia teknolojia ya kompyuta ,kuwanasa wahalifu mbalimbali badala ya kutumia mbinu za kizamani za kutumia vitisho na maguvu hivyo kuweza kukabiliana na wimbi la uhalifu nchini na mkoani hapa kwa ujumla na kuwataka wadau kushirikiana na jeshi hilo kufichua maovu.
Kamishina
Lusingu,amesema kutokana na kuwepo mbinu nyingi za kihalifu
zinazotumika jeshi la polisi nalo limebadili mfumo wa utendaji wake
ambapo sasa limejikita zaidi kwenye matumizi ya teknolojia kwa kutumia
Kompyuta kuwanasa wahalifu wanaofanya uhalifu eneo moja na kukimbilia
lingine ili kujificha.
Alisema
mfumo huo wa kutumia Kompyuta unarahisisha kuwatia mbaloni wahalifu
wowote wanaokimbilia eneo lingine kwa ajili ya kujificha baada ya
kufanya uhalifu.
Kuhusu
ajira, Mnadhimu huyo, amesema mfumo wa kuajiri askari umebadilika
ambapo sasa wanachukuliwa vijana kutoka vyuoni na sekondari ,badala ya
utaratibu wa zamani wa kutumia ngazi za kata na kuendelea na mchujo hadi
ngazi ya mkoa.
Kamanda,
Lusingu,amesema mfumo huu unamanufaa makubwa ambapo sasa watapatikana
askari waadilifu zaidi tofauti na mfumo uliokuwa ukitumika ambapo
baadhi yaaskari wanakuwa hawana uadilifu.
Kuhusu
vimo vya baadhi ya askari kuwa wenye maumbo madogo na wengine wafupi,
Lusingu, amesema maumbo sio tatizo bali watu wanaajiriwa kutokana na
utaalamu na elimu yao ,na kubwa wa maumbo ya miili ni mbinu iliyotumika
wakati wa ukoloni kwa ajili ya kutishia watu sasa hivi polisi wanafanya
kazi kwa kutumia elimu na sio maguvu.
Awali
akifungua kikao hicho mkuu wa dawati la jinsia la jeshi la polisi mkoa
wa Arusha, Mrakibu mwandamizi, Mary Lugora, amesema kuwa usalama wa
Arusha hauwezi kuwa endelevu kama hazitachukuliwa hatua za wananchi
kushirikiana na jeshi la polisi .
Lugora,
ambae pia ni mwenyekiti wa kamati ya ulinzi shirikishi mkoa wa
Arusha,alisema swala la usalama lina gharama kubwa hivyo ni jukumu la
kila mwananchi kushiriki kikamilifu katika kuimarisha ulinzi na usalama
kwenye maeneo mbalimbali kuanzia kwenye makazi yao.
’’Mfano
mzuri ni kwenye maonyesho ya sikukuu ya wakulima nane nane ambayo
yamemalizika hivi karibuni ambapo hapakutokea uhalifu na hiyo ni
kutokana na jinsi tulivyokuwa tumejipanga na tumefanikiwa kuwadhibiti
hivyo nina wahakikishia kuwa amani ya jiji la Arusha imerejea’’alisema
Lugora.
Mwenyekiti
huyo,Lugora,alisema jeshi la polisi linaendelea kujipanga ili
kukabiliana na mbinu mbalimbali za uhalifu na hivyo kuhakikisha jiji la
Arusha na mkoa kwa ujumla vinabakia kuwa salama na hivyo kuwezesha
wananchi na wawekezaji kuishi kwa usalama na kufanya shughuli zao bila
ya matatizo.
Kwa
upande wake mkuu wa polisi wilaya ya Arusha,OCD, mrakibu Francis duma,
akitoa mada kwenye kikao hicho kuhusu umuhimu wa kuimarisha ulinzi
shirikishi, amesema kuwa kila mmoja anapaswa kulinda mali yake na ya
taifa.
Alisema
mbinu ya kutumia doria ,kuwahi kwenye matukio na upelelezi pekee
hazitoi jawabu la kumaliza matatizo ya uhalifu bali msingi mkubwa ni
kufanya kazi kwa karibu na jamii ambao wanawafahamu wahalifu wakiwemo
majambazi.
‘’Uhalifu
sasa unafanyika kwa njia za kitaalamu kutokana na kupanuka kwa
teknolojia hivyo jeshi hilo nalo linatumia mbinu za kisasa na kuachana
taratibu na mbinu za kizamani ambazo ni sawa na ulinzi wa jadi ‘’alisema
duma.
Kamanda
duma,alisema, jeshi la polisi pekee haliwezi kulinda kila mwananchi kwa
sababu polisi waliopo nchini ni wachache sana ukilinganisha na idadi ya
wananchi ambao ni zaidi ya milioni 45.
Awali
katibu wa kamati ya ulinzi shirikishi jiji la Arusha, Adolf Olomi,
alisema lengo la kikao hicho ni kufahamiana, kuondoa pengo la
kutokuaminiana kati ya jeshi la polisi na wananchi, kuweka mkakati wa
kuimarisha ulinzi kwa kushirikiana kati ya polisi na jamii.
A;isema
swala la usalama na ulinzi halichagui mtu,hivyo lazima jeshi la polisi
liimarishe ushirikiano na jamii katika kuimarisha ulinzi na usalama wa
wananchi na mali zao na kujenga kuaminiana .
Maoni
Chapisha Maoni