Jaji Makame afariki dunia
.jpg)
Jaji Lews Makame
LIYEKUWA Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC),Jaji mstaafu Lews Makame, amefariki duniagazeti la Mtanzania limeripoti kwamba Jaji makame alifariki dunia jana katika Hospital ya AMI Trauma Center,iliyoppo Masaki jijini Dar es salaam alipokuwa akitibiwa.
Mtanzania linaendelea kusema kuwa mara baada ya kupatikana kwa taarifa hizo lilifika nyumbani kwa marehemu Masaki ambako mmoja wa watoto Wa marehemu aliwafukuza waandishi wa habari huku akitoa sharti kwa chombo kinachotaka kuripoti msiba wa Baba yake,lazima kiwe na kibali cha Serikali.
Mtoto huyo wa marehemu baada ya kutoa kauli hiyo, aliwaamuru wanahabari kutoka nje ya nyumba hiyo na familia haiko tayari kuwaona wakati wote wa mazishi ya Jaji Makame.
kitendo hicho kiliibua malumbano makali kati ya mtoto huyo wa marehemu na ambae alitaka kuvunja kamera za wanahabari ili wasiweze kurekodi tukio hilo la msiba.-CHANZO MTANZANIA
Maoni
Chapisha Maoni