Hatimaye Rodriguez apokea tuzo

Hatimaye James Rodriguez ametuzwa tuzo la mfungaji bora.
Hatimaye mshambulzi wa Colombia
James Rodriguez aliyeduwaza ulimwengu kwa kufunga mabao mengi zaidi
katika kombe la dunia lililokamilika huko Brazil mwezi uliopita amepokea
tuzo lake la mfungaji mabao mengi '' Golden Boot''.
Rodriguez ambaye aliyetikisa wavu mara 6 huko
Brazil sasa anakibarua cha kutafuta namba huko Real Madrid dhidi ya
wakinzani wenye haiba yake kama mchezaji bora msimu huu Christiano
Ronaldo.Mshambulizi huyo mwenye umri wa miaka 23 alisema kuwa anamatumaini makubwa ya kutamba Santiago Bernabéu
Maoni
Chapisha Maoni