Ghana katika hatari ya marufuku ya FIFA


Mashabiki wa Ghana

Ghana inakabiliwa na tishio la kupigwa marufuku na shirikisho la soka duniani FIFA baada ya serikali kuanzisha uchunguzi wa matokeo duni katika kombe la dunia huko Brazil.
The Black stars ya Ghana ilimaliza na alama moja pekee katika kundi G baada ya kucheza mechi tatu .

Aidha kampeini yao huko Brazil ilikumbwa na misukosuko ya nidhamu na migomo ya malimbikizi ya marupurupu ya wachezaji.
FIFA imeipatia onyo shirikisho la soka la Ghana kuikumbusha kuwa inakiuka kanuni za shirikisho hilo kwa kuruhusu au kushiriki uchunguzi wa aina yeyote kuhusiana na matokeo duni katika mchuano wa kombe la dunia iliyofanyika huko Brazil.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HADITHI:MWALIMU MAGDALENA sehemu ya 1

Hadithi: Mwalimu Magdalena sehemu ya 5

Hadithi: Mwalimu Magdalena sehemu ya 4