Ebola bado ni Tishio

Mkurugenzi wa madaktari hao wasio na mipaka Brice de la Vigne,ameeleza namna ugonjwa wa Ebola na unavyoenezwa unavyochukuliwa ni sawa na hakuna juhudi yoyote ama kwakifupi ni sifuri kiutendaji kwa wadau hao wakuu .
Kufuatia shutuma hizo shirika la Afya duniani haikukaa kimya na hivyo walisimama na kujitetea, na hivyo msemaji wa W.H.O alisema shirika lake limejitahidi kuongeza idadi ya wahudumu wa afya na mipango pamoja na usambazaji wa wataalamu hao katika maeneo yaliyoathiriwa na ugonjwa huo,hivyo si kweli kwamba hawajafanya kitu chochocte.
Shirika hilo la Afya ulimwenguni W.H.O limetoa takwimu ya watu waliopoteza maisha kutokana na ugonjwa wa Ebola Africa Magharibi kwamba kufikia sasa inazidi kuongezeka na kufikia zaidi ya wafu elfu kumi na watatu.-bbc
Maoni
Chapisha Maoni