DRC waendelea kuyakimbia makazi yao

'K/Kaskazini DRC waendelea kuyakimbia makazi yao'
Raia wa maeneo ya Kivu Kaskazini katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo wameendelea kuyakimbia makazi yao kutokana na ukosefu wa amani katika maeneo hayo.

Ofisi ya Uratibu wa Masuala ya Kibinadamu ya Umoja wa Mataifa katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo imetangaza kuwa, maelfu ya raia wa maeneo ya Walikale na Lubero katika mkoa wa Kivu Kaskazini mashariki mwa nchi hiyo wameyakimbia makazi yao kutokana na kuendelea kushuhudiwa machafuko na ukosefu wa amani katika mkoa huo.
Taarifa zaidi zinasema kuwa, raia hao kila siku wanaonekana wakiondoka katika makazi yao na kukimbilia katika maeneo mengine wakihofia usalama wa maisha yao.

Mchafuko yanayosababishwa na waasi wa kundi la FDLR kutoka Rwanda katika mkoa wa Kivu Kaskazini ndiyo sababu ya kuu inayowalazimisha raia kukimbia maeneo hayo.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HADITHI:MWALIMU MAGDALENA sehemu ya 1

Hadithi: Mwalimu Magdalena sehemu ya 5

Hadithi: Mwalimu Magdalena sehemu ya 4