Aliyepona Ebola akimbiwa na kutengwa

Aliyekufa kwa ebola azikwa
Wakati virusi vya Ebola
vikiendelea kusambaa katika Afrika Magharibi na kusababisha taharuki
miongoni mwa wakazi wa nchi zilizokwisha kuathirika na ambazo bado
hazijaathirika katika ukanda huo, baadhi ya walioupata gonjwa huo
wamepona lakini pamoja na kupona bado hiyo haiwafanyi kukwepa
kunyanyapaliwa.
Mmoja ya wanafunzi wa udaktari ambaye amepona
ugonjwa wa Ebola na kupewa cheti cha kuruhusiwa na kituo kilichokuwa
kikimpa matibabu huko nchini mwake Guinea lakini amejikuta katika wakati
mgumu kurudi katika maisha yake ya kawaida kwa kuwa watu wanamkimbia
ikiwemo shule anayosoma wakimwambia abaki nyumbani."Tunanyanyapaliwa na unajua wanapotutizama kama hivyo, unajua, hata familia yangu, watu wananitenga. Ninajisikia mpweke, wakati mwingine ninaenda matembezini. Ninaishi na Mjomba, wazazi wangu wanaishi kijijini. Nyumbani niko peke yangu, ninakula peke yangu na ninapohisi mambo hayako sawa ninaenda kutembeatembea. Shuleni wameniambia nikae nyumbani nitibiwe. Niko nyumbani tangu nilipoumwa. Siwezi kupata hata mahali pa kufanyia mazoezi yangu ya masomo kivitendo," Amesema mwanafunzi huyo
Maoni
Chapisha Maoni