Ajali yaua watu 15 Tabora

Watu 15 wamefariki dunia na wengine zaidi ya 75 kujeruhiwa vibaya baada ya mabasio mawili waliyokuwa wakisafiria kugongana mkoani Tabora.
Ajali hiyo ilitokea jana saa 10.00 jioni katika kijiji cha Mrogoro kilichoko Wilaya ya Sikonge mkoani humo,
Taarifa zilizo patikana kutoka eneo la tukio zinasema ajali hiyo ilihusisha mabasi mawili ya abiria.
Mtanzania rimeripoti kuwa mmoja wa mashuhda wa ajali hiyo aliye zungumza na mtanzania kwa simu kwa sharti la kuto kutajwa jina,aliyataja mabasi mabasi yaliyohusika na ajali hiyo kuwa ni basi la Kampuni ya AM lenye namba T 803 ATN ana basi la Kampuni ya Sabena lenye namba T 110 ARV.

"Lile basi la AM lilikuwa likitoka Mwanza kwenda Mpanda na lile la sabena lilikuwa likitoka Mbea kwenda Mwanza.
Yalipofka katika Kijiji cha Mrogoro majia kama ya saa 10.05jioni, yaligongana uso kwa uso, yaani ajali ni mbaya kwani dereva wa Sabena aliyetambuliwa kwa jina la James Kombe, amefariki dunia papo hapo baada ya kukatika kichwa.ambapo hadi muda Mtanzania inaripoti habari hii dereva wa basi la AM alikuwa bado hakitambui kwahiyo hata jina lake lilikuwa bado halijatambulika
Kuhusu majeruhi,walikimbizwa katika Hospitali ya Wilaya ya Sikonge kwaajili ya kupatiwa matibabu na hata ile miili ya waliopoteza maisha zilipelekwa hospitalini hapo kwaajili ya kuhifadhiwa,"
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora, Suzani Kaganda,alipotafutwa kwasimu yake ya mkononi kuzungumzia akali hiyo haikupatikana.-Chanzo Mtanzania aug 20

 
Baadhi ya miili ya marehemu.
 

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HADITHI:MWALIMU MAGDALENA sehemu ya 1

Hadithi: Mwalimu Magdalena sehemu ya 5

Hadithi: Mwalimu Magdalena sehemu ya 4